FT: Simba 2-1 Geita Gold FC.... Banda afungua akaunti ya magoli Simba SC..

>FT: Simba 2-1 Geita Gold FC.... Banda opens Simba SC goals account ..


Winger Peter Banda scored his first competitive goal with our squad in a 2-1 victory over Geita Gold held at Benjamin Mkapa Stadium in Dar es Salaam today.

Banda gave us the goal in the ninth minute after finishing off a cross from Kibu Denis from the right.

After the goal Geita came on top wanting to equalize but our defensive line down with Kennedy Juma and Joash Onyango was careful.

Mzamiru Yassin gave us the second goal in the 56th minute finishing off a free kick by Bernard Morrison just seconds after coming off the bench.

In 66 minutes Juma Mahadhi gave Geita the first goal following our central defenders negligently clearing the danger.

Coach Pablo Franco replaced Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Medie Kagere and Pascal Wawa to replace Ibrahim Ajibu, Rally Bwalya, John Bocco, Banda and Kibu.

This result has brought us to 17 points after playing seven matches winning five and drawing two.


Winga Peter Banda amefunga bao lake la kwanza la mashindano akiwa na kikosi chetu katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.

Banda alitupatia bao hilo dakika ya tisa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kibu Denis kutoka upande wa kulia.

Baada ya bao hilo Geita walikuja juu kutaka kusawazisha lakini safu yetu ya ulinzi iliyokuwa chini na Kennedy Juma na Joash Onyango ilikuwa makini.

Mzamiru Yassin alitupatia bao la pili dakika ya 56 akimalizia mpira wa faulo iliyopigwa na Bernard Morrison sekunde chache baada ya kuingia kutoka benchi.

Dakika 66 Juma Mahadhi aliipatia Geita bao la kwanza kufuatia walinzi wetu wa kati kuzembea kuondoa hatari.

Kocha Pablo Franco aliwaingiza Bernard Morrison, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Medie Kagere na Pascal Wawa kuchukua nafasi za Ibrahim Ajibu, Rally Bwalya, John Bocco, Banda na Kibu.

Matokeo haya yametufanya kufikisha alama 17 baada ya kucheza mechi saba tukishinda mitano na sare mbili.

Post a Comment

0 Comments