Pablo: Mpaka sasa Simba SC inacheza asilimia 5 tu ya staili ninavyotaka icheze...

>Pablo: So far Simba SC is playing only 5% of the style I want to play, there is a lot more work to do


Head Coach of Tanzania Mainland Football Champions Simba SC Pablo Franco Martin has said he is still building his squad to get the first team.

Coach Pablo has made the statement, after witnessing his team play two competitive games since he was handed the role of Chief of the SC SC Technical Bench.

Simba SC beat Ruvu Shooting 3-1 in the Tanzania Mainland Premier League on Friday (November 19) at CCM Kirumba Stadium in Mwanza, then beat Red Arrows 3-0 in the Confederations Cup knockout stage.

The Spanish coach said: "We are playing with a competitive team. So far it is only 5 percent, the team I want as a coach. I think in two months you will see the team I want. I tell you no African team will want to play with the team I make."

Coach Pablo was hired by Simba SC, following the departure of French coach Didier Gomes at the end of October, after the club were knocked out of the African Champions League, 3-1 against Jwaneng Galaxy of Botswana, at Benjamin Mkapa Stadium in Dar es salaam.

Before the game Simba SC beat Jwaneng Galaxy in Gaborone-Botswana 2-0.


 Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Pablo Franco Martin amesema bado anakijenga kikosi chake ili kupata kikosi cha kwanza.

Kocha Pablo ametoa kauli hiyo, baada ya kukishuhudia kikosi chake kikicheza michezo miwili ya ushindani tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la Simba SC.

Simba SC iliifunga Ruvu Shooting Mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Ijumaa (Novemba 19) Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kisha ikaichapa Red Arrows Mabao 3-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya mtoano.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema: “Tunacheza huku tunaitengeneza timu ya Ushindani, Mpaka sasa ni asilimia 5 tu, timu ninayoitaka mimi kama kocha, Nadhani baada ya miezi miwili mtaiona timu ninayoitaka, Nawaambia hakuna timu Afrika itatamani kucheza na timu ninayoitengeneza.”

Kocha Pablo aliajiriwa Simba SC, kufuatia kuondoka kwa Kocha kutoka Ufaransa Didier Gomes mwishoni mwa mwezi Oktoba, baada ya klabu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kabla ya mchezo huo Simba SC iliifunga Jwaneng Galaxy mjini Gaborone-Botswana mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments