Simba SC kucheza dhidi ya TP Mazembe kwenye tamasha la Simba Day

>Simba SC to play against TP Mazembe at the Simba Day festival


At the Simba Day Festival, our team will play with five-time African Champions League champions TP Mazembe from the Democratic Republic of Congo (DRC).

Simba's Chief Executive Officer, Barbara Gonzalez has confirmed tonight that TP Mazembe will be Simba's guests this time around.

“I am happy to announce to the Simba Fan's and all Tanzanians in general that we will play with TP Mazembe on Simba Day on September 19 this year.

"We have already completed all the procedures for inviting them and now it is official that they will be our guests," said Barbara.

She said TP MAzembe is one of the most respected teams in Africa and it is a great honor for Simba to get the opportunity to play with it here in the country.

Barbara said it was the goal of the leadership and technical bench to ensure the Simba get a good team to find out exactly where the squad for this season is in preparation for the upcoming league season.

In Africa, Mazembe is considered one of the best clubs and its name is associated with success in football.

More information about the arrival of Mazembe will continue to be provided by the club towards Simba Week and finally Simba Day.


Simba SC kucheza dhidi ya TP Mazembe kwenye tamasha la Simba Day


Katika Tamasha  la Simba Day, timu yetu itacheza na mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amethibitisha usiku huu kwamba TP Mazembe ndiyo watakuwa wageni wa Simba safari hii.

“Nina furaha kuwatangazia Wanasimba na Watanzania wote kwa ujumla kwamba tutacheza na TP Mazembe siku ya Simba Day Septemba 19 mwaka huu.

” Tayari tumekamilisha taratibu zote za kuwaalika na sasa ni rasmi kwamba wao ndiyo watakuwa wageni wetu,” amesema Barbara.

Amesema TP MAzembe ni mojawapo ya timu zenye heshima kubwa barani Afrika na ni heshima kubwa kwa Simba kupata fursa ya kucheza nayo hapa nchini.

Barbara amesema lilikuwa lengo la uongozi na benchi la ufundi kuhakikisha Simba inapata timu nzuri ili kujua ni wapi hasa kikosi cha msimu huu kipo kwenye maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Barani Afrika, Mazembe inachukuliwa kama mojawapo ya vilabu bora na jina lake linahusishwa na mafanikio katika mpira wa miguu.

Taarifa zaidi kuhusu ujio wa Mazembe zitaendelea kutolewa na klabu kuelekea katika Wiki ya Simba na hatimaye Simba Day.

Post a Comment

0 Comments