Simba Queens kucheza tena dhidi ya Lady Doves kutafuta mshindi wa tatu

>


Simba Queens to play against Lady Doves for a third winner


Our Women's team squad, Simba Queens will meet Lady Doves FC in a match to find a third winner in the Caf Women's Champions L
eague Cecafa Qualifiers 2021 to be played at Nyayo Stadium, September 9 at 7pm.

The teams were in Group A where when we met the game was fierce and ended in a goalless draw.

We lost the semi-final match against Vihiga Queens of Kenya when Lady Doves were beaten by Commercial Bank of Ethiopia on penalties 5-4.

Our match tomorrow will be exciting as the first match in the group stage ends in a draw where tomorrow's match must be won by one team.


Simba Queens uso kwa uso tena na Lady Doves mshindi wa tatu


Kikosi cha timu yetu ya Wanawake, Simba Queens itakutana na Lady Doves FC katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu katika mashindano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021 utakaopigwa Uwanja wa Nyayo, Septemba 9 saa saba mchana.

Timu hizo zilikuwa kundi A ambapo tulipokutana mchezo ulikuwa mkali na ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na kutinga nusu fainali.

Tulipoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Vihiga Queens ya Kenya wakati Lady Doves walifungwa na Commercial Bank of Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mchezo wetu wa kesho utakuwa ni wa kusisimua kutokana na mechi ya kwanza kwenye hatua ya makundi kumalizika kwa sare ambapo mechi ya kesho lazima timu moja ipate ushindi.

Post a Comment

0 Comments