Rasmi...Hizi ndio jezi za Simba SC kwa msimu huu...Uongozi waionya Yanga

>Official: Our jerseys for this season have been launched today


Tanzania Football Champions Simba SC in collaboration with the club's jersey sales partner, has decided to release new jerseys for the 2021/22 season, today Friday September 03.

Simba SC and Vunja bei (Company Vunja Bei) announced that tomorrow Saturday (September 04) will be the official launch day of the club's jerseys and will start selling them that day.

Acting Simba SC Information Officer Ezekiel Kamwaga spoke to reporters earlier today in Dar es Salaam, saying the need for Simba club jerseys from fans and members has prompted them to drop them the day before.

"Requests for jerseys from Simba fans have been huge and the management has seen fit to listen to them. I officially announce that from now on new Simba jerseys are now available at Vunja Bei stores nationwide ”said Ezekiel Kamwaga.

Regarding reports of the leak of Simba SC jerseys, and the decision to release them before the official launch date was announced earlier, Kamwaga said he could not confirm the matter, although he acknowledged in today's world that the issue is possible.

However, Kamwaga has rebuked the behavior of some people who dared to make dirty tricks of leaking jerseys, saying they are creating animosity that will not help Tanzanian football which has begun to take international action.

"There are teams like Coastal Union that have launched jerseys but they have not leaked, it has come to Simba the jersey has been leaked. This is a bad habit. If we start with the 'traditional joke' of leaking jerseys, when we go it will be a war. ” said Kamwaga.

However, the leadership of Simba SC, has emphasized the activities of introducing new jerseys, in a special event to be held in Dar es Salaam tomorrow Saturday.


Rasmi:Jezi zetu kwa msimu huu zimezinduliwa leo


Mabingwa wa Soka Tanzania  Simba SC kwa kushirikiana na Mbia wa  Uuzaji wa jezi za klabu hiyo, umeamua kuziachia jezi mpya za msimu 2021/22, leo Ijumaa Septemba 03.

Simba SC na Vunja bei (Kampuni Vunja Bei) walitangaza kuwa kesho Jumamosi (Septemba 04) kuwa siku ramsi ya uzinduzi wa jezi za klabu hiyo na kuanza kuziuza siku hiyo.

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, na kusema uhitaji wa jezi za klabu ya Simba kutoka kwa Mashabiki na Wanachama umewafanya kuziachia siku moja kabla.

“Maombi ya jezi kutoka kwa mashabiki wa Simba yamekuwa makubwa sana na uongozi umeona ni vyema kuwasikiliza. Natangaza rasmi kwamba kuanzia sasa jezi mpya za Simba zinapatikana sasa kwenye maduka ya Vunja Bei nchi nzima” amesema Ezekiel Kamwaga.

Kuhusu taarifa za kuvuja kwa Jezi za Simba SC, na kuepelekea maamuzi ya kutangaa kuziachia kabla ya tarehe rasmi ya uzinduzi iliyokua imetangaza awali, Kamwaga amesema hawezi kuthibitisha suala hilo, japo amekiri katika ulimwengu wa sasa suala hilo linawezekana.

Hata hivyo Kamwaga amekemea tabia ya baadhi ya watu waliothubutu kufanya njama chafu za kuvujisha jezi, kwa kusema wanatengeneza uhasama ambao hautalisaidia soka la Tanzania ambalo limeanza kupiga hatua kimataifa.

“Kuna timu kama Coastal Union wamezindua jezi lakini hazikuvuja, imefika Simba jezi imevuja. Hii ni Tabia mbaya. Tukianza ‘utani wa jadi’ wa kuvujisha jezi, Tunapokwenda itakuwa ni vita.” amesema Kamwaga.

Hata hivyo Uongozi wa Simba SC, umesisitiza shughuli za kutambulisha jezi mpya, katika hafla maalum itakayofanyika jijini Dar es salaam kesho jumamosi.

Post a Comment

0 Comments