Kanoute, Onyango warejesha matumaini Simba SC..Mpango mzima uko hivi..

>Kanoute, Onyango restore hope to Simba SC


Three Simba SC stars, Joash Onyango, Sadio Kanoute and Jonas Mkude, are likely to be part of the squad that will play against Dodoma City, tomorrow Friday at the Jamhuri Stadium, Dodoma.

That is after missing out on Tuesday's Tanzania Premier League match against Biashara United played at Karume Stadium in Musoma. The stars are missing for a variety of reasons, including injuries and family problems.

According to the team's co-ordinator, Abbas Ally, Onyango, Kanoute missed the game against Biashara due to injuries sustained in the Community Shield match against Yanga played at Mkapa Stadium, Dar.

Ally said the players have recovered from their injuries and may travel with the team to Dodoma for the game against Dodoma City which will be played tomorrow Friday at the Republic Stadium.

He added that midfielder Jonas Mkude has ended family problems while Thadeo Lwanga ended up serving a red card he received in the Community Shield game, so he will be part of the squad that will play against Dodoma.

"In our first league game we have missed four players due to various problems including injuries, family problems and card penalties.

“The players are Onyango, Kanoute, Mkude and Lwanga who are all key players and dependents in our Simba squad.

"The players including the injured Onyango and Kanoute have recovered, Mkude has ended family problems while Lwanga is finishing his red card, so they will join the team in Dodoma region for the Dodoma City game," said Ally.


NYOTA watatu wa Simba SC, Joash Onyango, Sadio Kanoute na Jonas Mkude, huenda wakawa sehemu ya kikosi hicho kitakachocheza dhidi ya Dodoma Jiji, kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Hiyo ni baada ya kukosekana katika mchezo wa Jumanne wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Biashara United uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume huko mjini Musoma. Nyota hao wamekosekana kwa sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na matatizo ya kifamilia.

Kwa mujibu wa mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally, Onyango, Kanoute waliukosa mchezo dhidi ya Biashara kutokana na majeraha waliyoyapata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ally alisema kuwa wachezaji hao wamepona majeraha yao na huenda wakasafiri na timu kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Jamhuri .

Aliongeza kuwa kiungo Jonas Mkude amemaliza matatizo ya kifamilia wakati Thadeo Lwanga akimaliza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, hivyo atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Dodoma.


Post a Comment

0 Comments